DAMASCUS, Syria
WAPIGANAJI wa kundi la kigaidi la IS nchini Syria wametoroka gerezani wakati vikosi vya jeshi la Serikali vikipigana na waasi wa SDF.
Taarifa zinaeleza kuwa mapigano hayo yalitokea jana Januari 19, 2026, na magaidi 1,500 wa IS walinufaika nayo kwa kutoroka katika Gereza la Shaddadeh.
Kabla ya kuzuka upya kwa mapigano, tayari kulikuwapo na mazungumzo ya kumaliza tofauti iliyopo kati ya Serikali na waasi nchini humo.
Mazungumzo hayo yaliwahusisha Rais wa mpito wa Syria, Ahmad al-Sharaa, na kiongozi wa wapiganaji wa SDF, Mazloum Abdi.
Hata hivyo, baada ya mazungumzo ya pande mbili hizo, Abdi hakueleza walichokubaliana na upande wa Serikali.
Hata hivyo, chanzo kimoja cha habari kilidai kuwa mazungumzo hayo hayakwenda vizuri.


