10.5 C
New York

Madrid kung’oa kiungo Chelsea?

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Real Madrid inampigia hesabu kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez, ikipanga kukamilisha usajili huo ifikapo mwishoni mwa msimu huu wa 2025-26.

Madrid inataka mchezaji wa eneo la kiungo na itakumbukwa kwa mwaka jana walikaribia kumnasa Martin Zubimendi, kabla ya nyota huyo kutua Arsenal akitokea Real Sociedad.

Kwa sasa, matajiri hao wa La Liga wameelekeza nguvu zao kwa Fernandez, pia ikielezwa kuwa Chelsea wako tayari kufanya biashara.

Taarifa zinaeleza kuwa Blues wanasikilizia ofa ya maana kutoka kwa klabu yoyote inayomtaka nyota huyo mwenye umri wa miaka 25.

Fernandez raia wa Argentina, alijiunga na Blues mwaka 2023 akitokea Benfica ya Ureno, ambapo usajili wake uligharimu kitita cha Pauni milioni 106.8.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img