MADRID, Hispania
IMERIPOTIWA kuwa mabosi wa Real Madrid wameanza kumfikiria kocha aliyetimuliwa Chelsea hivi karibuni, Enzo Maresca.
Wakati huo huo, Rais wa Madrid, Florentino Perez, ametajwa kutamani usajili wa mpachikaji mabao wa Manchester City, Erling Haaland.
Kwa upande wa kocha, mbali ya Maresca, bado zipo taarifa zinazodai kuwa Madrid haijaacha kuwafikiria Jurgen Klopp na Zinedine Zidane.
Xabi Alonso alifungashiwa virago muda mfupi tu baada ya Madrid kufungwa mabao 3-2 na wapinzani wao, Barcelona, katika mchezo wa Spanish Super Cup.
Wakati huu Alvaro Arbeloa akiwa amepewa majukumu ya muda, Perez amekuwa na kibarua cha kusaka kocha atayeiongoza Madrid.
Kwa upande wa Klopp ambaye amekuwa nje ya kazi ya ukocha kwa muda mrefu, inaelezwa kuwa Mjerumani huyo havutiwi kwenda Santiago Bernabeu.
Pia, Zidane anasubiri kumrithi Didier Deschamps atayejiuzulu kuinoa timu ya taifa ya Ufaransa baada ya fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia.


