10.5 C
New York

Man United yamkomalia Baleba

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KLABU ya Manchester United imeendelea kukazia harakati zake za kumsajili kiungo wa Brighton na timu ya taifa ya Cameroon, Carlos Baleba.

Man United ilijaribu kumsajili ‘mido’ huyo mwenye umri wa miaka 20 dakika za mwisho za usajili uliopita wa majira ya kiangazi, mwaka jana.

Hata hivyo, dili hilo liligonga mwamba baada ya uongozi wa Brighton kuitaka iweke mezani kitita cha Pauni milioni 100.

Baada ya kusikia Brighton wameshusha dau na kufikia Pauni milioni 80, Man United imerejea katika mbio za kumsajili nyota huyo.

Hatua ya Brighton kushusha dau imetokana na kuporomoka kwa kiwango cha mchezaji huyo, ambapo hajafunga wala kutoa ‘asisti’ katika mechi 19 alizocheza msimu huu.

Kwa sasa, changamoto kubwa iliyobaki kwa Man United ni upinzani mkali kutoka kwa klabu zingine zinazomtaka Baleba, ikiwamo Manchester City.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img