8.4 C
New York

Man United yaitandika City, Carrick aendeleza rekodi

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KATIKA mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa Old Trafford leo Januari 17, 2026, Manchester United chini ya kocha mpya, Michael Carrick, imeifunga Manchester City mabao 2-0.

Huko ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Carrick tangu alipokabidhiwa majukumu ya kuinoa Man United hadi mwishoni mwa msimu huu.

Hivyo, kiungo huyo wa zamani wa ‘Mashetani Wekundu’ ameendeleza rekodi yake ya kufanya vizuri katika mechi alizowahi kupewa kwa muda benchi la ufundi.

Ikumbukwe, alipopewa mikoba baada ya Ole Gunnar Solskjaer kufukuzwa mwaka 2021, alishinda mechi mbili na kutoa sare moja.

Kwa mchezo wa leo, Man United iliyomtimua kocha Ruben Amorim siku chache zilizopita ilipata mabao yake kupita kwa Bryan Mbeumo (dk. 65) na Patrick Dorgu (dk. 76).

Huenda ingekuwa siku mbaya zaidi kwa Pep Guardiola na vijana wake wa Man City kama si mabao ya Amad Diallo na Bruno Fernandes kukataliwa kipindi cha kwanza.

Baada ya mechi hiyo, Carrick alisema: “… Tulitaka kucheza vizuri leo, tulitaka kujitoa kwa ajili ya mchezo huu. Tulitaka kuwa bora kwenye ulinzi na nadhani pia tulikuwa hatari katika ushambuliaji.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img