10.5 C
New York

Chelsea, City zagombea kinda Barcelona

Published:

LONDON, Uingereza

CHELSEA imeungana na Manchester City na Borussia Dortmund zinazoiwania saini ya mshambuliaji chipukizi wa Barcelona, Dro Fernandez.

Fernandez (18), anataka kuondoka Barcelona na hatua yake hiyo imeelezwa kuibua mvutano mkubwa katika uongozi wa klabu hiyo.

Baadhi ya mabosi wa klabu hiyo hawakubaliani na uamuzi wake, wakisema nyota huyo ni miongoni mwa makinda bora kuwahi kuzalishwa na ‘academy’ yao ya La Masia.

Awali, Dortmund ndiyo iliyokuwa mstari wa mbele na kupewa nafasi kubwa zaidi ya kuinasa huduma ya Fernandes lakini Chelsea na Man City nazo zimevamia.

Habari njema kwa klabu hizo ni kwamba mkataba wa ‘dogo’ huyo una kipengele kinachomruhusu kuondoka Camp Nou kwa ada ndogo tu ya euro milioni 6.

Katika hatua nyingine, maskauti wa PSG na Bayern Munich nao wameripotiwa kuimezea mate saini ya Fernandes.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img