10.5 C
New York

Arsenal macho kwa ‘Pedri wa Serbia’

Published:

LONDON, Uingereza

WASHIKA Bunduki wa London, Arsenal, wanampigia hesabu kiungo wa kimataifa wa Serbia, Vasilije Kostov, ambaye uchezaji wake unafananishwa na ule wa staa wa Barcelona, Pedri.

Kostov mwenye umri wa miaka 17, anaitumikia Red Star Belgrade ya Serbia na ni miongoni mwa makinda wanaotabiriwa makubwa katika soka la Ulaya.

Nyota huyo ameshahusika katika mabao 11 msimu huu, akiwa amecheza mechi 27. Kwamba amefunga mabao sita na kutoa ‘asisti’ tano.

Gazeti la Sun limeripoti kuwa kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, alianza kumtolea macho kinda huyo tangu wakati wa usajili wa kiangazi wa mwaka jana.

Arteta anavutiwa na uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi katika eneo la kiungo. Mbali ya kuwa kiungo wa ulinzi na kati, pia Kostov anaweza kutokea pembeni (winga).

Red Star wanaweza kugoma kumwachia Januari hii lakini watahitaji Pauni milioni 17 kumfungulia mlango wa kutokea mwishoni mwa msimu huu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img