8.4 C
New York

Simba yabeba kocha Mamelodi

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KLABU ya Simba imeliimarisha benchi lake la ufundi kwa kumuajiri aliyekuwa kocha wa U-19 ya Mamelodi Sundowns, Kristopher Bergman.

Bergman mwenye umri wa miaka 36, ni chaguo la kocha Steve Barker, ambaye ameomba aajiriwe ili awe msaidizi wake.

Kocha mpya huyo ana leseni B ya Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) na aliwahi kuwa mchezaji wa Barker wakiwa Stellenbosch FC ya Afrika Kusini mwaka 2019.

Akiwa mchezaji, pia Bergman aliwahi kuzitumikia klabu zingine kadhaa za Ligi Kuu ya nchi hiyo, zikiwamo Chippa United na All Stars.

Kwa msimu mmoja tu aliokaa kwenye benchi akiwa kocha, aliiwezesha U-19 ya Mamelodi kutwaa ubingwa wa Ligi ya vijana ya Afrika Kusini.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img