8.4 C
New York

Ligi Kuu Bara 2025-26 … Dodoma Jiji v Singida Black Stars

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

NI Ijumaa, Januari 16, 2026, ambapo timu hizo zitakutana zikiwa ‘zinapumulia mashine’ msimu huu wa Ligi Kuu Bara. Dodoma Jiji, wenyeji wa mchezo, wako nafasi ya 15 kwenye msimamo, huku Singida Black Stars wakiwa ya 12.

Baada ya kushuka dimbani mara nane, Dodoma wao wana pointi sita, wakati Singida wao wamekusanya pointi nane baada ya mechi zao tano.

Katika mechi zao tano, Singida wameshinda mbili, wamefungwa moja na kuambulia sare mbili. Mabao ya kufunga ni manne, huku wakiwa wameruhusu manne.

Kwa upande wao, Singida haijapata ushindi katika mechi tano za hivi karibuni, zikiwamo za kimataifa. Imefungwa mbili na kupata sare tatu.

Dodoma Jiji imeshinda moja, imefungwa nne na kutoa sare tatu katika mechi nane za Ligi Kuu ilizocheza msimu huu.

Pia, haijapata ushindi katika mechi tano zilizopita; imefungwa mara tatu na kutoa sare mbili. Ilitoa suluhu na Mashujaa katika mchezo uliopita.

Licha ya kufunga mabao manne, safu yao ya ulinzi imeonekana kuwa tatizo kubwa, ambapo imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara tisa.

Rekodi za mechi tatu ilizocheza dhidi ya Dodoma Jiji zinaonesha kuwa Singida imeshinda mbili na kufungwa moja.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img