LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Bukayo Saka, amekubali kuongeza mkataba wa miaka mitano klabuni hapo.
Saka, ambaye amekuwa mchezaji muhimu kikosini katika miaka ya hivi karibuni, amesaini akiwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa sasa.
Hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa England ataendelea kuwatumikia Washika Bunduki hao wa London hadi mwaka 2031.
Tangu alipotokea timu za vijana klabuni hapo mwaka 2018, Saka amekuwa na mchango mkubwa katika eneo la ushambuliaji la Arsenal.
Msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL), staa huyo mwenye umri wa miaka 24 ameshaifungia mabao manne na kutoa asisti tatu.


