WASHINGTON DC, Marekani
RAIS wa Marekani, Donald Trump, ameionya Iran akiiambia ataingilia kati, ikiwamo kuivamia kijeshi, endapo itaendelea kuua waandamanaji.
Watu nane wameripotiwa kupoteza maisha kwa kipindi cha wiki moja ya maandamano makubwa ya raia wanaoipinga Serikali nchini Iran.
Hasira za raia hao zinatokana na hali mbaya ya kiuchumi, achilia mbali kashfa za rushwa zinazoiandama Serikali.
Kwa upande wake, Rais Trump amedai kuwa Marekani haitasubiri endapo vyombo vya dola vya Iran havitaacha kuua raia.
Kupitia taarifa yake katika mitandao ya kijamii, amesema: “Kama Iran inawapiga risasi waandamanaji, ambao wanatekeleza utamaduni wao, Marekani itaingilia kati kuwasaidia.”
Hata hivyo, mshauri wa kiongozi wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameitaka Marekani kuwa makini na mpango wake huo wa kuingilia yanayoendelea nchini mwao.


