15 C
New York

Marekani yaishambulia Venezuela, yamdaka Maduro

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

RAIS Donald Trump amethibitisha kuwa wanajeshi wake wameishambulia Venezuela na kumkamata kiongozi wa Taifa hilo, Nicolas Maduro.

Wakati huo huo, Rais Trump amedai kuwa si Maduro pekee, bali hata mkewe anashikiliwa na wanajeshi wa Marekani.

Hatua hiyo imekuja baada ya wiki kadhaa za uhusiano mbaya kati ya mataifa hayo, ambapo Trump amekuwa akimshutumu Maduro kujihusisha na mtandao wa biashara ya dawa za kulevya.

Kabla ya Trump kutangaza kumkamata, taarifa za awali zilidai kuwa Maduro aliondoka Venezuela na kukimbilia kusikojulikana.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kile alichokieleza Rais Trump, wamemtia nguvuni ‘adui’ yake huyo baada ya kumkuta akiwa na mkewe kwenye makazi yao.

Tukio la vikosi vya Marekani kuingia Venezuela na ‘kumchomoa’ Maduro linafananishwa na lile la mwaka 1989, ambapo waliivamia Panama na kumchukua aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Manuel Noriega.

Maduro na Noriega wana historia inayofanana juu ya uhusiano wao na Marekani, wakitajwa na Taifa hilo kujihusisha na biashara ya ‘unga’ (dawa za kulevya).

Lakini, tofauti na ilivyotokea kwa Maduro, kukamatwa kwa Noriega kulikuja baada ya vita kali ya Panama na Marekani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img