22 C
New York

Rais Taiwan aitangazia vita China

Published:

TAIPEI, Taiwan

KATIKA salamu zake za Mwaka Mpya wa 2026, Rais wa Taiwan, Lai Ching-te, amejiapiza kuilinda nchi yake dhidi ya uvamizi wa China.

China imekuwa ikiitaja Taiwan kuwa ni sehemu ya eneo lake na kusisitiza uwezekano wa kukivamia Kisiwa hicho.

Kwa siku mbili mfululizo, vikosi vya kijeshi vya China viliendesha programu ya mazoezi ya kivita maeneo ya jirani na Taiwan.

Ifahamike kuwa hatua ya China kufanya hivyo ilikuja baada ya Marekani kuipatia Serikali ya Taiwan kiasi cha Dola bilioni 11.1 ili kuimarisha jeshi.

Hata hivyo, katika hotuba yake ya jana Desemba 31, 2025, Rais Ching-te amesema: “Nikiwa kama Rais, msimamo wangu haujawahi kubadilika. Ni kusimama na kulinda uhuru wa taifa.

“Ni kuimarisha ulinzi wa taifa na utulivu wa jamii nzima, bila kusahau kujenga misingi imara ya Kidemokrasia.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img