Na Mwandishi Wetu, Gazetini
TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘ Taifa Stars’ imefuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya AFCON 2025 kama ‘best loser’ baada ya leo kutoka sare ya bao 1-1 na Tunisia.
Star iliyokuwa kundi C imemaliza katika nafasi ya tatu na alama mbili, imeungana na Nigeria na Tunisia waliofuzu moja kwa moja katika kundi hilo.
Taifa Stars ilianza michuano hiyo kwa kufungwa 2-0 na Nigeria, kisha kutoka sare ya 1-1 na Uganda na leo kutimisha na Tunisia.
Uganda ambao walikuwa katika kundi hilo wamemaliza safari yao baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Nigeria.


