18 C
New York

Serikali yamkalia kooni bilionea Chelsea

Published:

LONDON, Uingereza

SERIKALI ya Uingereza imemtaka mmiliki wa zamani wa Chelsea, Roman Abramovich, kuchagua kati ya kuichangia Ukraine kiasi cha Pauni bilioni 2.5 au kukubali kufunguliwa mashitaka.

Agizo linataka bilionea huyo wa Urusi kuchota kiasi hicho katika fedha alizovuna baada ya kuiuza Chelsea mwaka 2022.

Abramovich ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa Urusi, ambao mali zao zilishikiliwa kama adhabu kwa kitendo cha Taifa lao kuivamia Ukraine.

Kama itakumbukwa, ni kutokana na presha hiyo, ndipo mfanyabiashara huyo alipolazimika kuiweka sokoni klabu yake ya Chelsea.

Sasa, Serikali ya Uingereza inawataka kuchagia fedha za kuisaidia Ukraine kufanya marekebisho ya miundombinu yake iliyoathiriwa na mashambulizi ya Urusi.

Kwa upande wake, Abramovich amesema fedha zinachangwa zinapaswa kwenda pia nchini Urusi kwani hata nchi hiyo imeathiriwa na vita dhidi ya Ukraine.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img