18 C
New York

Bayern hesabu zote kwa Fernandes

Published:

MUNICH, Ujerumani

VIGOGO wa soka la Ujerumani, Bayern Munich, wanavutiwa na mpango wa kumsajili nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes.

Fernandes mwenye umri wa miaka 31, katika mahojiano yake ya wiki chache zilizopita, aliibua kauli iliyoashiria kuwa atatimka Old Trafford.

Katika mahojiano yake, kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno alisema wapo baadhi ya *¨¨M wa Man United hawataki abaki klabuni hapo.

Alisema wakurugenzi hao walitaka aondoke wakati wa usajili uliopita wa majira ya kiangazi lakini kocha Ruben Amorim alizuia mpango huo.

Wakati huo, Fernandes alikuwa akihusishwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu ya Saudi Arabia, ikiwamo Al-Hilal iliyotenga ofa nono ya Pauni milioni 100.

Kwa sasa, staa huyo ana mkataba na Man United utakaokwisha mwaka 2027 na una kipengele kinachomruhusu kuongeza miezi 12 hapo baadaye.

Katika hatua nyingine, mtandao wa TalkSPORT umeripoti kuwa baadhi ya wachezaji wa Man United wanaamini Fernandes atawaacha msimu huu utakapokwisha.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img