15 C
New York

Urusi yatangaza kuteka mji Ukraine

Published:

MOSCOW, Urusi

SERIKALI ya Urusi kupitia kwa Msemaji wake, Dmitry Peskov, imetangaza kile ilichokiita kuwa ni ushindi baada ya kuteka mji ulioko Mashariki wa Donetsk, Ukraine. Kwa mujibu wa Peskov, Mji waliofanikiwa kukuchukua ni Pokrovsk ambao ameuita kuwa ni eneo muhimu kwa ‘maadui’ zao hao.

Kuthibitisha hilo, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imeweka video kwenye ukura wake wa mtandao wa kijamii wa Telegram ikiwaonesha wanajeshi wake wakiwa kwenye mitaa ya mji walioutaja kuwa ni Pokrovsk.

Hata hivyo, hakuna kiongozi wa Ukraine aliyeibuka na kuthibitisha kuwa Mji wao huo umeangukia kwenye mikono ya Urusi. Aidha, hayo yanatokea wakati tayari Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, ameshakutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron.

Ifahamike kuwa msingi wa mazungumzo yao ni namna ya kurejesha utulivu nchini Ukraine kwa kumaliza mgogoro wao na Urusi. Kabla ya hapo, wawakilishi wa Ukraine walifanya mazungumzo na Marekani, ajenda ikiwa ni hiyo hiyo.

Licha ya Marekani kusema yapo matumaini makubwa ya kurejesha utulivu, hatua ya Urusi kuendelea kuchukua maeneo ya Ukraine inatafsiri safari ndefu iliyopo katika kuyapatanisha mataifa hayo ya Mashariki mwa Ulaya.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img