15 C
New York

UN: Watu 300,000 wamekimbia makazi Msumbiji

Published:

MAPUTO, Msumbiji

UMOJA wa Mataifa (UN) umekiri kupata wasiwasi juu ya machafuko yanayoendelea Kaskazini mwa Msumbiji na kudai kuwa watu takribani 300,000 wamekimbia makazi yao. Machafuko hayo yanayotokana na mapigano kati ya vikundi vya waasi na Serikali yameripotiwa zaidi katika Jimbo la Cabo Delgado, ambalo limeshuhudia vifo vya watu zaidi ya 6,200.

Kile kilichoelezwa na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) ni kwamba watu takribani 100,000 wamekimbia makazi kwa kipindi cha wiki mbili tu zilizopita. Kwa kipindi cha miezi mitatu ya hivi karibuni, watu zaidi ya 287,000 wamekimbia makazi yao, kwa mujibu wa mwakilishi wa UNHCR, Xavier Creach.

“Naweza kusema idadi hiyo ni ya watu waliosajiliwa tu. Naweza kusema watu zaidi ya 300,000 wamekimbia makazi tangu Julai (mwaka huu),” amesema.

Tangu mwaka 2017, vikundi mbalimbali vya waasi vimekuwa vikivamia na kushambulia vijiji, pia vikizuia misaada ya kibinadamu kuingia maeneo mengi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img