15 C
New York

Mgombea urais anusurika kuuawa

Published:

LIMA, Peru

MGOMBEA urais katika Uchaguzi Mkuu wa Peru unaotarajiwa kufanyika Aprili, mwakani, Rafael Belaunde, amenusurika kuuawa katika shambulio la risasi. Belaunde alishambuliwa na watu wasiojulikana akiwa kwenye gari na dereva wake huko Kusini mwa Mji Mkuu wa Lima.

Wakiwa kwenye pikipiki, watu hao walianza kulishambulia kwa risasi gari la mwanasiasa huyo aina ya SUV, ingawa si yeye wala dereva wake aliyeuawa. Katika tukio hilo, Belaunde mwenye umri wa miaka 50 alijeruhiwa kidogo usoni kutokana na vioo vilivyovunjika.

Katika maelezo yake kwa polisi, hakuwahi kupokea jumbe za kutishiwa maisha kabla ya hicho kilichotokea.
Ifahamike kuwa Belaunde ni miongoni mwa wanasiasa maarufu nchini Peru kwani aliwahi kuwa Waziri wa Nishati.

Muasisi huyo wa Chama cha Libertad Popular (Popular Liberty), anatokea familia ya siasa kwani babu yake, Fernando Belaunde, aliwahi kuwa rais wa Peru kwa mihula miwili.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img