15 C
New York

Maelfu waandamana wakitaka Serikali ijiuzulu

Published:

SOFIA, Bulgaria

MAANDAMANO makubwa yameibuka katika Jiji la Sofia, Bulgaria, ambapo maelfu ya wananchi wameingia barabarani wakishinikiza Serikali kujiuzulu. Taarifa za awali juu ya maandamano hayo zinaeleza kuwa watu 10 wanashikiliwa na vyombo vya dola, huku polisi watatu wakijeruhiwa.

Hoja ya msingi ya waandamanaji hao ni kupinga bajeti ya Serikali ya mwaka 2026, ambayo inaelekeza kupandisha kodi. Pia, wanapinga vitendo vya rushwa kwa ujumla. Wafuatiliaji wanakiri kuwa maandamano hayo ni makubwa zaidi kuwahi kutokea katika miaka mingi ya hivi karibuni.

Katika maeneo ya katikati mwa Mji Mkuu wa Sofia, waandamanaji zaidi ya 50,000 wameonekana wakiwa nje ya jengo la Bunge la nchi hiyo. Wengi kati ya waandamanaji hao walikuwa na bendera za Bulgaria na Umoja wa Ulaya, pia wakisema Serikali ya Rais Rosen Zhelyazkov inapaswa kujiuzulu.

Bulgaria, ambayo ni nchi ndogo barani Ulaya ikiwa na watu milioni 6.4, ni moja ya zile zenye kiwango kikubwa cha rushwa katika taasisi zake za umma. Kwa mujibu wa takwimu, katika nchi 27 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Ulaya, Bulgaria imezidiwa na Hungary pekee katika zile zinazotawaliwa na vitendo vya rushwa.
“Tupo hapa kupigania kesho yetu. Tunataka kuwa nchi ya Ulaya, siyo nchi inayoongozwa kwa rushwa na kundi la Mafia (kundi la kihalifu),” alisema mmoja ya waandamanaji, Ventsislava Vasileva.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img