10.7 C
New York

Alonso mbioni kutimuliwa Madrid

Published:

MADRID, Hispania

ENDAPO Xabi Alonso hakutakuwa na mabadiliko katika mechi chache zijazo, mabosi wa Real Madrid watamfuta kazi kocha wao raia wa Hispania, Xabi Alonso. Madrid imeendelea kupata matokeo yasiyoridhisha katika mechi zake za hivi karibuni, ikiwamo sare ya bao 1-1 dhidi ya Girona wikiendi iliyopita.

Ikumbukwe, hiyo ilikuwa ni sare ya tatu mfululizo kwenye Ligi baada ya kugawana pointi na Rayo Vallecano na Elche katika michezo miwili iliyopita.

Kwa upande wao, si tu kukosa ushindi, bali pia mabosi wa Madrid hawakufurahishwa na kitendo cha kuiona timu yao ikijilinda kwa dakika 10 za mwisho za ushindi wao wa mabao 4-3 dhidi ya Olympiacos.
Katika Ligi, mara ya mwisho kwa Madrid kupata ushindi ilikuwa Novemba Mosi, mwaka huu, walipoifunga Valencia mabao 4-0 katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Vyanzo vya ndani katika klabu ya Madrid vinaeleza kuwa viongozi hawavutiwi na kiwango cha timu yao katika siku za hivi karibuni na mechi chache zijazo zinaweza kuamua hatima ya Alonso.

Wakati huo huo, bado zimekuwapo taarifa zinazodai kuwa chanzo cha Madrid kutokufanya vizuri ni uhusiano mbaya kati ya Alonso na baadhi ya wachezaji klabuni hapo. Gazeti la Marca la Hispania linawataja mastaa sita wasiovutiwa na kocha huyo ni Vinicius Jr, Jude Bellingham, Fede Valverde, Rodrygo, Brahim Diaz, Endrick na Ferland Mendy.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img