MERSEYSIDE, Uingereza
MSHAMBULIAJI mpya wa Liverpool, Florian Wirtz, huenda akatimka klabuni hapo ifikapo Januari, mwakani.
Licha ya feha nyingi zilizotumika kumng’oa Bayern Leverkusen, Wirtz ameshindwa kung’ara Anfield, ambapo hana bao wala ‘asisti’ tangu asajiliwe.
Ni kutokana na takwimu hizo, ni kama kocha Arne Slot ameamua ‘kumpotezea’ kwani hamtumii kwenye kikosi cha kwanza.
Taarifa zinaeleza kuwa Liverpool inataka kumtoa kwa mkopo nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani.
Wakati ikipiga hesabu za kumtoa kwa mkopo, Liverpool imeendelea kuhusishwa na mpachikaji mabao wa Bournemouth, Antoine Semenyo.
Published:


