15 C
New York

Ramos aachana na mabosi wake Mexico

Published:

MEXICO City, Mexico
BEKI wa zamani wa Real Madrid, Sergio Ramos, ameachana na klabu yake ya Rayados inayoshiriki Ligi Kuu ya Mexico.
Ramos, ambaye pia alikuwa nahodha Santiago Bernabeu, ameondoka klabuni hapo baada ya kumaliza mkataba wake.
Hata hivyo, licha ya umri wake wa miaka 39, bado Ramos raia wa Hispania haoneshi nia ya kustaafu soka.
Alijiunga na Rayados mwanzoni mwa mwama huu, ikielezwa kuwa alisaini mkataba wa muda mfupi tu.
Akiwa na kikosi hicho, nyota huyo wa zamani wa PSG alicheza mechi 21 na kufunga mabao matatu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img