MANCHESTER, England
MABOSI wa Manchester City wamemuweka kwenye rada zao kiungo wa kimataifa wa England, Elliot Anderson.
Kwa mujibu wa taarifa, Man City inavutiwa na mchezaji huyo na sasa inasubiri dirisha dogo la usajili la Januari, mwakani.
Mtandao wa Mail Sport umeeleza kuwa si tu Mkurugenzi, Hugo Viana, bali hata kocha Pep Guardiola ni shabiki wa mchezaji huyo.
Kwa mujibu wa ripoti, Viana amekuwa akifuatilia mechi za Nottingham Forest ili kumuona nyota huyo mwenye umri wa miaka 22.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa huenda isiwe rahisi kwa Forest kumwachia Januari, na badala yake ikasubiri amalize msimu huu.
Forest, kwa mujibu wa taarifa zilizopo, watamwachia endapo watawekewa mezani kitita cha Pauni milioni 80.
Anderson ni ‘kiraka’ kwani ukiacha kiungo wa ulinzi (namba 6), pia amekuwa akicheza kwa ustadi mkubwa anaposogea katika eneo la kiungo wa kati (namba 8).
Published:


