12.6 C
New York

Sobhi afungiwa miaka minne kucheza soka

Published:

CAIRO, Misri
KIUNGO wa zamani wa Stoke City na Huddersfield Town, Ramadan Sobhi, amefungiwa kucheza kandanda kwa kipindi cha miaka minne.
Nyota huyo raia wa Misri mwenye umri wa miaka 28, ameshukiwa na rungu hilo baada ya kubainika kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
Sobhi alitua Ligi Kuu ya England mwaka 2016, alipojiunga na Stoke City akitokea Al Ahly.
Wakati huo, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa klabu za Misri aliyesajiliwa nje ya nchi kwa fedha nyingi, euro milioni 5.
‘Messi wa Misri alisajiliwa ili kuwapa ushindani wa namba waliokuwa mastaa wa timu hiyo, Xherdan Shaqiri na Marko Arnautovic.
Hata hivyo, baada ya adhabu hiyo, mwanasheria wake ameweka wazi kuwa mpango uliopo ni kukata rufaa.
Kwa upande wake, Sobhi hajazungumza chochote juu ya taarifa hizo za kufungiwa kucheza soka.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img