12.6 C
New York

‘Mashemeji Derby’ bado kizungumkuti Kenya

Published:

NAIROBI, Kenya
KUNA uwezekano mkubwa wa ‘derby’ kubwa zaidi Ligi Kuu ya Kenya kati ya Gor Mahia na AFC Leopards ikapigwa kalenda kwa mara nyingine.
‘Mashemeji Derby’ ilitarajiwa kuchezwa Jumamosi ya wiki hii lakini inaelezwa kuwa sakata la kukosekana kwa uwanja linaweza kuifanya ikasogezwa mbele.
Awali, mechi hiyo ilitarajiwa kuchezwa Novemba 30, mwaka huu, kabla ya kurudishwa nyuma na kupangwa kufanyika siku moja kabla (Novemba 29).
Hata hivyo, sasa zipo taarifa kuwa Uwanja wa Taifa wa Nyayo uliotarajiwa kutumika umechukuliwa kwa matumizi ya Serikali, hivyo haitawezekana kwa mechi hiyo kuchezwa hapo.
Taarifa zinaeleza kuwa Uwanja huo uko kwenye maandalizi ya hafla ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani inayotarajiwa kufanyika Desemba Mosi, mwaka huu.
Mechi hiyo ingeweza kupelekwa katika Uwanja wa Moi Kasarani lakini tayari klabu ya Nairobi United itautumia kwa mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya AS Maniema Union ya DRC.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img