MANCHESTER. Uingereza
MABOSI wa Manchester United wameanza harakati za kumshawishi kiungo wake, Casemiro, asaini mkataba mpya klabuni hapo.
Hata hivyo, ushawishi huo unaenda sambamba na mabosi wa Man United kumuomba Mbrazil huyo apunguze mshahara.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33, amekuwa kwenye kiwango bora kwa siku za hivi karibuni, licha ya awali kuonekana amekwisha.
Katika hatua nyingine, Man United bado inampigia hesabu winga wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo.
Ripoti zinaelez kuwa ‘Mashetani Wekundu’ hao wa Old Trafford watajaribu kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ifikapo Januari, mwakani.
Published:


