RIYADH, Saudi Arabia
SOKA la Saudi Arabia limejizolea umaarufu mkubwa katika miaka ya hivi karibuni. Taifa hilo linashika nafasi ya 60 kwa ubora duniani.
‘The Green’ ni mabingwa mara tatu wa Kombe la Asia, wakifanikiwa kutwaa taji la michuano hiyo katika miaka ya 1984, 1988 na 1996.
Kikosi chao kimekuwa chini ya kocha wa kimataifa wa Ufaransa, Herve Renard, ambaye amekuwa mwajiriwa tangu Julai, 2019.
Renald, kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’, aliiongoza Morocco katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018.
Pia, kikosi kina mastaa Firas Al Buraikan (Al Ahli), Salem Al Dawsari (Al Hilal) na Musab Al Juwayr (Al Qadsiyah). Al Buraikan alifunga mabao matano katika mechi za kufuzu.
Saudi Arabia walitikisa fainali zilizopita za Kombe la Dunia za mwaka 2022 baada ya kuifunga Argentina mabao 2-1 katika mchezo wa hatua ya makundi.
Hata hivyo, safari yao kwenye mashindano hayo iliishia hatua hiyo ya makundi baada ya kupoteza mechi mbili dhidi ya Poland na Mexico.
Hii itakuwa mara ya tatu mfululizo kwa Saudi Arabia kufuzu Kombe la Dunia. Kwa ujumla, ni mara yao ya saba kushiriki mashindano hayo lakini ni mara moja tu (1994) waliyofanikiwa kuvuka makundi.
Published:


