10.2 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Norway (31)

Published:

OSLO, Norway
KWA mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia, mashabiki wa soka watamshuhudia straika wa viwango, Erling Haaland, akicheza michuano hiyo.
Norway imefuzu na inashika nafasi ya 29 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Kikosi chao kinanolewa na kocha Stale Solbakken, ambaye amekuwa kwenye benchi la ufundi tangu alipoajiriwa Desemba, 2020.
Solbakken ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Norway na alikuwa sehemu ya kikosi kilichocheza Kombe la Dunia mwaka 1998.
Haaland anayekipiga Ligi Kuu ya England akiwa na Manchester City alifanya kazi kubwa kuiwezesha Norway kufuzu fainali zijazo kwani alifunga mabao 16.
Ni kwa maana hiyo, sasa nyota huyo amefikisha mabao 55 katika mechi 48 alizocheza tangu alipoanza kuitumikia Norway.
Ukimuweka kando Haaland, kikosi cha Norway kina wachezaji wengine wanaocheza klabu kubwa barani Ulaya. Miongoni mwao ni Alexander Sorloth (Atletico Madrid) na Oscar Bobb (Man City).
Wamerejea Kombe la Dunia baada ya kuikosa michuano hiyo kwa miaka 28. Mara ya mwisho kwa Norway kucheza fainali hizo ilikuwa mwaka 1998.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img