14 C
New York

Odegaard fiti kuivaa Tottenham

Published:

LONDON, Uingereza
KIUNGO wa Arsenal, Martin Odegaard, amepona majeraha yake na huenda akaikabili Tottenham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England wa Jumapili ya wiki hii.
Ikumbukwe, Odegaard ambaye ni nahodha wa kikosi, amekosekana katika mechi saba za hivi karibuni kutokana na majeraha ya goti.
Kwa mujibu wa taarifa, nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 ameshapona na kuanza mazoezi, hivyo atacheza ‘derby’ hiyo ya London.
Kurejea kwake kunaweza kumpunguzia msongo wa mawazo kocha Mikel Arteta kwani huenda akamkosa Viktor Gyokeres aliyeumia mwanzoni mwa mwezi huu.
Odegaard hakucheza lakini alikuwa na timu yake ya taifa ya Norway katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia, ambapo walikata tiketi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998.
Staa huyo aliingia uwanjani kuungana na wenzake kushangilia baada ya dakika 90 za mchezo walioifunga Estonia mabao 4-1.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img