15 C
New York

Mane afunguka alivyoikataa Man United

Published:

MANCHESTER, England
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Senegal, Sadio Mane, amesema alikataa ofa ya Manchester United kabla ya kutua Liverpool.
Mane alijiunga na Liverpool mwaka 2016 kwa ada ya Pauni milioni 30, ambapo aliifungia mabao 120 katika mechi 269.
Akiwa Liverpool, alitengeneza ‘pacha’ kali ya ushambuliaji akishirikiana na Mohamed Salah na Roberto Firmino, kabla ya kuondoka na kutua Bayern Munich mwaka 2022.
Akizungumzia alivyosajiliwa na Liverpool, Mane amesema alianza kupokea ofa ya Man United, wakati huo ikiwa chini ya kocha Louis van Gaal.
Kwa mujibu wa Mane, aliona ingekuwa ngumu kwake kupata nafasi ya kuanza mbele ya Wayne Rooney, Angel Di María na Memphis Depay.
“Waliposhindwa kunisajili, ndipo walipomsajili [Anthony] Martial,” amesema Mane.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img