CATALUNYA, Hispania
KATIKA kitabu chake kipya, straika wa Barcelona, Robert Lewandowski, amefichua alivyoitwa na mabosi wa klabu hiyo na kumuomba asifunge mabao.
Kupitia kitabu hicho kiitwacho kinachoitwa ‘Lewandowski: The Real One’, staa huyo anasema hilo lilitokea katika msimu wake wa kwanza Camp Nou.
Lewandowski mwenye umri wa miaka 37, alijiunga na Barca mwaka 2022 akitokea Bayern Munich, usajili uliogharimu kiasi cha Pauni milioni 42.5.
Sasa, kwa kuwa katika mkataba wao na Bayern kulikuwa na kipengele kinachoitaka Barca kulipa Pauni milioni 2.2 endapo Lewandowski angefikisha mabao 25 katika msimu wake wa kwanza, mabosi wa Barca ‘wakajiongeza’.
Kwa mujibu wa Lewandowski, aliitwa na mabosi wa klabu hiyo, akiwamo Rais Joan Laporta, na kuombwa asifunge tena baada ya mabao 23 aliyokuwa nayo.
Kama itakumbukwa, ni msimu ambao nyota huyo alifunga mabao 23 katika mechi 34 za Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).
Published:


