18 C
New York

Rooney ataja watatu anaowakubali EPL

Published:

MANCHESTER, Uingereza
MKONGWE wa Manchester United, Wayne Rooney, amewataja wachezaji watatu wanaomvutia msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Akihojiwa hivi karibuni, Rooney alianza kwa kumtaja mshambuliaji wa Bournemouth, Antoine Semenyo, ambaye amefunga mabao sita na kutoa ‘asisti’ tatu katika mechi 11.
“Nafikiri ni mchezaji mzuri sana kwa Bournemouth, akiendeleza kiwango bora alichokuwa nacho msimu uliopita,” alisema Rooney.
Katika nafasi ya pili, lejendari huyo amemuweka staa wa Bryan Mbeumo, akisema: “Nafikiri amekuwa mchezaji mzuri kwa Man United, hata baada ya kuanza vibaya katika siku zake za mwanzo klabuni hapo. Nafikiri ni mchezaji mzuri sana.
Pia, Rooney amemtaja mshambuliaji wa Arsenal raia wa Sweden, Viktor Gyokeres. “Arsenal walikuwa wakilia kwa miaka mingi kwa kukosa straika. Amekuja na ufanisi wake ni wa kiwango cha juu, ingawa hajafunga mabao mengi,” alisema.
Hata hivyo, Rooney amekumbana na ukosolewaji mkubwa kutoka kwa mashabiki huko mitandaoni, wakiamini alipaswa kumuweka pia Erling Haaland.
Haaland ameshaifungia Manchester City jumla ya mabao 14 kwenye Ligi msimu huu na ametoka kuiwezesha timu yake ya taifa kufuzu Kombe la Dunia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img