RABAT, Morocco
BEKI wa kulia wa PSG na timu ya taifa ya Morocco, Achraf Hakimi, ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Shirikisho la Soka barani Afrika kwa Mwaka 2025.
Hakimi mwenye umri wa miaka 27, amekabidhiwa tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika mjini Rabat, Morocco.
Nyota huyo amewapiku mastaa wengine wawili, Mohamed Salah, na Victor Osimhen, baada ya kuipa PSG taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.
Katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo, alifunga bao la kwanza walipoifunga Inter Milan mabao 5-0.
Hakimi ameibeba tuzo hiyo baada ya kuikosa mara mbili mfululizo (2023 na 2024) na anakuwa nyota wa kwanza wa Morocco kuwa mshindi tangu mwaka 1998.
Wakati huo huo, Ghizlane Chebbak wa Morocco ametajwa kuwa ndiye Mchezaji Bora wa Mwaka huu kwa upande wa soka la wanawake.
Chebbak ameondoka na tuzo hiyo akiwapiku Rasheedat Ajibade wa Nigeria na mwenzake wa Morocco, Sanaa Mssoudy.
Published:


