18 C
New York

Gyan aitabiria Nigeria ubingwa AFCON

Published:

ACCRA, Ghana
MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan, anaamini Nigeria ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa fainali za AFCON zitakazoanza Desemba, mwaka huu.
Gyan aliyewahi kukipiga Sunderland ya England, pia akitwaa mara tatu ubingwa wa AFCON, amesema Nigeria itatumia fainali hizo kujipoza machungu ya kushindwa kufuzu Kombe la Dunia.
Wakati huo huo, Gyan hakuacha kuzitaja Ivory Coast na Morocco katika timu anazozipa nafasi kubwa ya kuwa mabingwa.
“Nigeria ilifanya vizuri msimu uliopita, walikaribia kutwaa ubingwa. Ivory Coast nao walifanya vizuri, tuna timu nyingi nzuri,” alisema.
“Ninaweza kusema Nigeria, Ivory Coast na Morocco ni chaguo langu katika zile zenye nafasi ya ubingwa kwa AFCON 2025.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img