15.2 C
New York

Kocha Nigeria: DRC walitumia uchawi kutufunga

Published:

RABAT, Morocco
BAADA ya timu ya soka ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’ kufungwa na DRC, kocha wake, Eric Chelle, ameibua shutuma nzito dhidi ya wapinzani wao.
Eagles walifungwa kwa penalti 4-3 katika mchezo huo wa ‘playoff’ wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwakani.
Mchezo huo uliochezwa mjini Rabat, Morocco, ulifika hatua ya penalti baada ya sare ya bao 1-1.
Sasa, baada ya mechi hiyo, kocha wa Eagles, Chelle, alidai kuwaona wachezaji wa DRC wakifanya vitendo vya ushirikiana.
Akizungumza kwa lugha ya Kifaransa, Chelle alisema wachezaji wa DRC walifanya hivyo wakati wa upigaji wa penalti.
Chelle mwenye umri wa miaka 48, alilalamika kuwa wachezaji wa DRC walikuwa wakiroga kila walipokuwa wakienda kupiga penalti.
“Katika penalti zote walizopiga, wachezaji wa Congo walikuwa wanafanya ushirikiana,” alisema kocha huyo.
Hata hivyo, kocha wa DRC raia wa Ufaransa, Sebastien Desabre, amepuuzia madai ya Chelle akisema hakuna ukweli wowote.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img