LONDON, Uingereza
KLABU ya Chelsea imeinasa saini ya kinda mwenye umri wa miaka 16 kutoka katika kikosi cha Independiente del Valle ya Ecuador, Deinner Ordonez.
Independiente del Valle ni klabu ya zamani ya kiungo wa sasa wa Chelsea, Moises Caicedo.
Hata hivyo, Ordonez atatua Stamford Bridge atakapotimiza umri wa miaka 18.
Nyota huyo anayecheza eneo la ulinzi ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha U-20 ya Ecuador.
Hivi karibuni, Chelsea wamekuwa na uhusiano mzuri na Independiente, ikikumbukwa kuwa ndiko anakotokea pia Estevao Willian.
Willian, licha ya umri wake mdogo wa miaka 18, amekuwa akimpa ushindani mkali wa namba Pedro Neto katika eneo la winga ya kulia.
Published:


