14 C
New York

Mashabiki waziponza Al Ahly, Zamalek

Published:

CAIRO, Misri
VURUGU za mashabiki wa Al Ahly na Zamalek katika ‘derby’ ya Super Cup zimesababisha klabu hizo kutozwa faini ya LE 100,000 (zaidi ya Sh mil. 10 za Tanzania) kila moja.
Katika mchezo huo, Al Ahly waliibuka wababe kwa ushindi wa mabao 2-0, wakitwaa ubingwa huo kwa mara ya 16.
Kwa upande mwingine, Zamalek wao wamekumbana na adhabu nyingine ya faini ya LE 100,000 kutokana na fujo za mashabiki wao katika mechi yao na Pyramids FC.
Pia, adhabu imemfikia kiungo wa pembeni wa timu hiyo raia wa Brazil, Juan Bezerra, na staa wa Al Ahly, Ahmed Sayed Zizo, ambao kila mmoja ametozwa faini ya LE 50,000 kwa kosa la kukataa kuwapa mkono waamuzi.
Wakati huo huo, kocha wa Pyramids FC, Krunoslav Jurcic, ametozwa faini ya LE 10,000 kwa kosa la kugoma kuzungumza na waandishi wa habari walipofungwa mabao 2-1 na Ceramica Cleopatra.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img