14 C
New York

Kane aingia rada za mabosi Barcelona

Published:

CATALUNYA, Hispania
MATAJIRI wa klabu ya Barcelona wanaangalia uwezekano wa kuinasa huduma ya mpachikaji mabao wa Bayern Munich, Harry Kane.
Mpango wa kumsajili Muingereza huyo umelenga kuziba pengo la Robert Lewandowski, ambaye kwa umri wake wa miaka 37, ni wazi anaelekea kumaliza soka lake.
Vyanzo mbalimbali vya habari barani Ulaya vinaeleza kuwa Barcelona wamepanga kuvunja mkataba wa Kane ifikapo Juni, mwakani, ambapo watalazimika kuilipa Bayern kiasi cha Pauni milioni 57.
Kane amekuwa moto wa kuotea mbali tangu alipotua Bayern mwaka 2023 akitokea ­Tottenham kwani ameshafunga mabao 108 katika mechi 113.
Mwezi uliopita, aliweka wazi kuwa mpango wake si kuondoka, bali kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Bundesliga.
Awali, Barcelona walitaka kumsajili moja kwa moja mshambuliaji wao wa mkopo kutoka Manchester United, Marcus Rashford, ambapo wangetumia Pauni milioni 30 tu kuvunja mkataba wake.
Hata hivyo, Rais wa Barcelona, Joan Laporta, hajavutiwa na kiwango cha Muingereza huyo na anataka kumrudisha Old Trafford mwishoni mwa msimu huu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img