LONDON, Uingereza
SHIRIKISHO la Soka la Ulaya (UEFA) limeshatangaza ratiba ya fainali zijazo za Mataifa ya Ulaya, maarufu kwa jina la ‘Euro 2028’.
Ratiba inaonesha kuwa Uwanja wa Principality wa mjini Cardiff, Wales, ndiyo utakaotumika kwa mchezo wa ufunguzi.
Wakati huo huo, Uwanja wa Wembley jijini London umekabidhiwa mechi za nusu fainali, pamoja na ile ya fainali.
Viwanja tisa vitatumika kwa kipindi chote cha mwezi mmoja wa michuano hiyo itakayofanyika Juni 9 hadi Julai 9, 2028, ambapo zitachezwa jumla ya mechi 51 hadi kufikia fainali.
Ifahamike kuwa wenyeji wa mashindano hayo ni England, Scotland, Wales na Jamhuri ya Ireland na yatashirikisha mataifa 24.
Timu ya taifa ya England ‘Three Lions’ itacheza mechi yake ya kwanza katika Uwanja wa Manchester City, Etihad, kabla ya kuhamia Wembley.
Ukiacha Man City, klabu zingine za Ligi Kuu ya England ambazo viwanja vyake vitatumika ni Tottenham, Aston Villa, Everton na Newcastle United.
Published:


