10.9 C
New York

Mke amtaka Oscar kuacha soka

Published:

RIO, Brazil
STAA wa zamani wa Chelsea, Oscar, huenda akatangaza kutundika daluga kutokana na ushauri wa mkewe na familia.
Oscar mwenye umri wa miaka 34, kwa sasa yuko kwenye chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kuanguka akiwa mazoezini kutokana na ugonjwa wa moyo.
Nyota huyo wa Sao Paulo ya Ligi Kuu ya Brazil, amekuwa akipatiwa matibabu ya moyo tangu Agosti, mwaka huu.
Licha ya kusema anaendelea vizuri, Gazeti la Globo la Brazil limeripoti kuwa Oscar ameshauriwa na mke kuachana na mchezo wa kandanda.
Nyota huyo aliwika England akiwa na Chelsea, kabla ya kutengeneza utajiri wa Pauni milioni 150 alipotimkia Ligi Kuu ya China.
Kwa sasa, Oscar ana mkataba na Sao Paulo utakaofikia ukomo mwaka 2027 lakini mabosi wa klabu hiyo wako tayari kumruhusu endapo ataamua kustaafu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img