10.9 C
New York

JKT Queens yalazimishwa sare, yaisubiri TP Mazembe

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Wanawake, JKT Queens, wamelazimishwa sare ya bao 1-0 na ASEC Mimosas.

Katika mchezo huo wa Kundi B uliochezwa katika Uwanja wa Right To Dream mjini Cairo, Misri, Ester Maseke aliitanguliza JKT Queens kwa bao la dakika ya 8. Hata hivyo, ASEC ya Ivory Coast ilicharuka na kusawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penalti ya dakika ya 82, mfungaji akiwa ni Erika Gnounoue.

Ni kwa matokeo hayo, sasa ASEC iko kileleni mwa msimamo wa Kundi B baada ya kufikisha pointi nne, ikifuatiwa na TP Mazembe yenye tatu, JKT Queens ikiwa na mbili, wakati Gaborone inaburuza mkia ikiwa na moja. Dhidi ya ASEC imekuwa ni sare ya pili kwa JKT Queens msimu huu, ambapo walipata matokeo ya aina hiyo pia katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Gaborone.

Hivyo, JKT Queens itavuka hatua ya makundi endapo itaifunga TP Mazembe katika mchezo wa Jumamosi ya wiki hii, siku ambayo ASEC watamenyana na Gaborone ya Botswana. Ikumbukwe, JKT Queens wanashiriki kwa mara ya pili mashindano hayo ya Shirikisho la Soka barani Afrika baada ya kuiwakilisha Tanzania mwaka 2023.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img