LISBON, Ureno
MPACHIKAJI mabao wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo, ameweka wazi kuwa fainali zijazo za Kombe la Dunia za mwakani zitakuwa za mwisho kwake kucheza soka.
Ureno haijafuzu lakini inahitaji ushindi tu dhidi ya Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa kesho.
Ronaldo ana umri wa miaka 40 na tayari ameshafunga mabao 953 kwa ngazi ya klabu na timu ya taifa.
Fainali za mwakani zitakazofanyika Canada, Mexico na Marekani zitakuwa za sita kwa Ronaldo kucheza katika maisha yake ya soka.
Akihojiwa na mjini Riyadh, Saudi Arabia, ‘CR7’ aliulizwa endapo anaona fainali zijazo zitakuwa ni mwisho kwake kucheza kandanda.
Akijibu, alisema: “Bila shaka. Nitakuwa na umri wa miaka 41 na nafikiri utakuwa wakati sahihi kupitia michuano hii mikubwa.”
Ronaldo anayekipiga Ligi Kuu ya Saudi Arabia akiwa na Al-Nassr, anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji pekee duniani aliyeifungia mabao mengi (143) timu ya taifa.
Mwaka 2006, aliiongoza Ureno kutwaa taji la fainali za Mataifa ya Ulaya (Euro), achilia mbali kwamba ana tuzo tano za Ballon d’Or.
Published:


