23.2 C
New York

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Published:

Na Winfrida Mtoi, Gazetini

Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na kufunga mabao katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya Asec Mimosa ya Ivory Coast  kwenye  michuano ya  Ligi ya Mabingwa Afrika inayoendelea katika jiji la Ismailia, Misri.

JKT Queens ambayo ni mwakilishi pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki katika michuano hiyo, itaivaa Asec Mimosa kesho Novemba 12, 2025. Mchezo wa kwanza ilikutana Gaborone United na kutoka sare ya bao 1-1.

Jamila amesema katika mchezo uliopita walikuwa na mapungufu katika eneo la mwisho, hali iliyochangia kushindwa kupanda ushindi licha ya kupata nafasi kadhaa za kufunga.

Amesema benchi la ufundi tayari limefanyia kazi mapungufu hayo kwa sasa kikosi kipo katika hali nzuri na wana malengo makubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Related articles

Recent articles