MANCHESTER, Uingereza
NAPOLI imeendelea kumfuatilia kiungo wa Manchester United, Kobbie Mainoo, ikipanga kumsajili kwa mkopo ifikapo Januari, mwakani.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 anataka kuondoka Old Trafford.
Napoli chini ya kocha wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte, inamuona Mainoo kuwa ni mchezaji atakayeifaa kwenye mbio za msimu huu wa Serie A na Ligi ya Mabingwa.
Mainoo anavutiwa na Napoli baada ya kuona mchezaji mwingine aliyeondoka Man United, Scott McTominay, anawika na vigogo hao wa Italia.
Napoli wanamtaka mchezaji huyo kwa mkopo, ingawa wako tayari kumlipa mshahara wote anaopokea Man United na kumsajili moja kwa moja hapo baadaye.
Kwa upande wake, Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis, amebariki usajili wa Mainoo akiamini atasaidia na Stanislav Lobotka kwenye eneo la kiungo.
Mbali ya Napoli, klabu zingine zinazomtolea macho nyota huyo ni Tottenham, Newcastle na Manchester City.
Published:


