23.2 C
New York

Tottenham yamfungia kazi Ndiaye

Published:

LONDON, Uingereza
KLABU ya Tottenham imeachana na mpango wa kumsajili Morgan Rogers wa Aston Villa, na sasa inamtaka winga wa Everton, Iliman Ndiaye.
Kwa mujibu wa taarifa, mabosi wa Spurs walimfukuzia Rodgers kwa muda mrefu lakini kocha mpya, Thomas Frank, havutiwi na mchezaji huyo.
Na badala yake, Frank anamtaka Ndiaye ambaye amekuwa na kikosi cha Everton tangu mwaka 2024 na amefunga mabao 15 katika mechi 49.
Hata hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa Senegal ana mkataba wa miaka minne na Everton, ambao utakwisha mwaka 2029.
Wakati huo huo, taarifa zingine zilizopo zinaeleza kuwa Rodgers ameshakubali kusaini mkataba mpya utakaombakiza Aston Villa.

Related articles

Recent articles