MANCHESTER, Uingereza
KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim, amesema atalazimika kutafuta straika mpya endapo Benjamin Sesko ataendelea na kusumbuliwa na majeraha ya goti.
Sesko alitokea benchi katika dakika ya 58 ya mchezo uliopita dhidi ya Tottenham lakini alidumu uwanjani kwa dakika 30 pekee, kabla ya kutolewa baada ya kuumia goti.
Kutolewa kwake kulisababisha Man United imaliza mchezo huo wa Ligi Kuu ya England ikiwa na wachezaji 10 kwani tayari ilishamaliza kufanya mabadiliko.
Baada ya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, Amorim alisema: “Ngoja tuone. Kuna shida alipata kwenye goti lake, ngoja tuone.”
Man United itakumbana na wakati mgumu kwenye eneo la ushambuliaji wakati Bryan Mbeumo, Amad na Noussair Mazraoui watakaporejea Afrika kushiriki fainali za Mataifa Afrika (AFCON) zitakazoanza Desemba, mwaka huu.
Published:


