MILAN, Italia
MABOSI wa Fiorentina wametangaza kumfuta kazi kocha wao, Stefano Pioli, kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo msimu huu wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A).
“ACF Fiorentina inathibitisha kwamba Stefano Pioli ameondoshwa kwenye majukumu ya kocha mkuu wa timu,” imeeleza taarifa ya klabu hiyo.
Fiorentina haijaonja ushindi msimu huu na sasa iko mkiani mwa msimamo ikiwa na pointi nne pekee baada ya kushuka dimbani mara 10.
Pioli alirejea Fiorentina mwaka huu ikiwa ni mara yake ya pili kuliongoza benchi la ufundi la timu hiyo.
Mechi ya mwisho akiwa kwenye benchi ni ile waliyotandikwa bao 1-0 na Lecce mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa, kocha wa U-19, Daniele Galloppa, amekabidhiwa kwa muda kibarua cha kuliongoza benchi la ufundi la timu ya wakubwa.
Published:


