23.2 C
New York

Arsenal wavunja rekodi ya mwaka 1903

Published:

LONDON, Uingereza
BAADA ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Slavia Prague usiku wa jana, sasa Arsenal imeandika historia ya kucheza mechi nane mfulululizo bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa.
Ni kwa maana hiyo, Arsenal wameivunja rekodi ya mwaka 1903, ambapo pia walifikisha mechi nane mfululizo bila kuruhusu bao.
Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa Jamhuri ya Czech, Arsenal walipata mabao hayo kupitia kwa Bukayo Saka (dk. 32) na Mikel Merino aliyeweka mawili (dk. 46 na 68).
Kwa upande mwingine, Washika Bunduki sasa wamefikisha ushindi wa mechi 10 mfululizo za mashindano mbalimbali msimu huu.
Katika hatua nyingine, nyota wa Arsenal, Max Dowman, ambaye ana umri wa miaka 15, ameandika historia ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kucheza Ligi ya Mabingwa.
Dowman aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Trossard, amevunja rekodi ya Youssoufa Moukoko aliyecheza Ligi ya Mabingwa akiwa na miaka 16.
Arsenal sasa wameshinda mechi zote nne walizocheza msimu huu wa Ligi ya Mabingwa. Wameshinda mechi zote 13 za mashindano mbalimbali walizocheza hivi karibuni.

Related articles

Recent articles