20.9 C
New York

Vinicius abisha hodi Ligi Kuu England

Published:

MADRID, Hispania
KITENDO cha Vinicius Junior kubwatukiana na kocha wake, Xabi Alonso, kimeibua taarifa kuwa nyota huyo ataondoka Real Madrid.
Vinicius mwenye umri wa miaka 25, alirushiana maneno na Alonso wakati wa mchezo wa El Classico dhidi ya Barcelona siku chache zilizopita.
Mshambuliaji huyo raia wa Brazil alikerwa na kitendo cha kutolewa zikiwa zimebaki dakika 20 za mchezo huo wa La Liga.
Taarifa zinaeleza kuwa Vinicius hafurahishwi na namna Alonso anavyomchukulia, hivyo yupo tayari kuondoka Santiago Bernabeu.
Katika mechi 316 tangu aliposajiliwa na Madrid, Vinicius amefunga mabao 111, likiwamo la ushindi uliowapa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2022.
Kama hiyo haitoshi, mwaka jana alipachika bao la ushindi katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Borussia Dortmund.
Kwa Ligi Kuu ya England, Chelsea na Manchester City zimekuwa zikiimezea mate huduma ya staa huyo anayelipwa Pauni 350,000 kwa wiki pale Madrid.

Related articles

Recent articles